Monday, November 4, 2013

vidonda vya tumbo na matibabu yake

Na Khamisi Ibrahim 

VIDONDA vya tumbo ni uharibifu wa kuta za ndani ya tumbo. Kwa maneno mengine, ni majeraha ndani ya tumbo. 

Vidonda vya tumbo vimegawanyika sehemu mbili; vidonda vya ndani ya tumbo (gastric ulcer) au sehemu ya juu ya utumbo mdogo (duodenal ulcer). 

Vidonda vinavyotokea katika utumbo ndivyo maarufu sana na huonekana zaidi kutokea kwa wanaume, na vidonda vya ndani ya tumbo huwashambulia wote wanaume na wanawake. Kutokana na tafiti za hivi karibuni, takribani mtu mmoja kati ya watu kumi atakuwa na vidonda vya tumbo. 

Vidonda vya tumbo hutokeaje mwilini? 

Chakula kinapoingia tumboni kwa ajili ya kusagwa, tumbo huzalisha majimaji mbalimbali, miongoni mwayo yaliyo muhimu zaidi ni asidi hidrokloriki. 

Asidi hii huanza kula kuta za tumbo/doudeni. Aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi. 

Utokeaji wa vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili. Kwanza, vitu ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua, vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, utumiaji pombe, chai, kahawa na baadhi ya dawa kama corticostisteroids, caffeine, reseprine, n.k. 

Pili, udhaifu wa ute au kuta za tumbo/duodeni kuzuia ushambuliaji wa asidi. Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kuongeza kinga ya ute au kupunguza uzalishaji wa asidi. 


Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha 

Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo. 

Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo imetengenezwa kwa ajili ya kukisaga chakula chochote haraka iwezekanavyo. 

Lakini kama hakuna chakula cha kufanyiwa kazi, asidi hii humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda. 

Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonesha kuwa akili hutumia biokemia katika mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangakia sana katika kutokeza kwa magonjwa mengi. 

Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu. 

Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili/mawazo yatokanayo na shida za maisha. 

Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, wenye kupewa talaka na wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa mara kutokana mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa. 

Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui. Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya tendo. 

Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe hadhiri zaidi, na hapo myunyizo wa adrenalini, homoni yenye nguvu huongezeka. 

Kadiri mfadhaiko unavyokuwa mfupi, ndivyo pia athari yake inavyokuwa fupi. Lakini pindi mfadhaiko unapokuwa mrefu, kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo, athari yake huendelea. 

Dalili za mfadhaiko 

Ikiwa bila ya sababu yoyote, zaidi ya dalili sita katika hizi zifuatazo zitatokea, basi mtu amwone daktari kuhusiana na mfadhaiko. 

Kujisikia huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote, kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi, kupoteza hamu ya tendo la ngono na kupoteza hamu ya chakula (au kula sana). 

Nyingine ni kukosa usingizi (au kulala sana), wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia pamoja, kushindwa falakinika, kushindwa kukumbuka na kushindwa kuamua, kughadhibishwa na vitu vidogo, kujiona huna thamani na kujitenga na marafiki na ndugu. 

Haraka haraka 

Haraka! Haraka! Lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda vya tumbo. Mbanano wa ratiba pia husababisha matumbo nayo kubanana. 

Malalamishi makubwa leo ya wagonjwa kwa madaktari wao ni: "Tumbo langu linanisokota na kuniletea matatizo, husikia kiungulia baada ya kula". Haraka na wasiwasi ni baadhi ya sababu ya matatizo haya. 

Tumbo ni kama kioo cha akili. Akili ikihangaishwa, basi wasiwasi na msukosuko wa hisia hufungia breki kwenye viungo vya ndani. Akili iliyohangaishwa na kukimbizwa mbio mbio hupeleka hisia kwenye tumbo na kusababisha mkazo wa ghafla wa misuli na hapo husababisha kiungulia na maumivu. 

Vyakula vya kusisimua 

Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo. Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile kachapu, haradali, achali, pilipili na vingine vingi huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni. Sababu ni kuwa, visisimuaji huchoma. Tumbo linahitaji kupozwa na si kusasuliwa. 

Dalili za vidonda vya tumbo 

Vidonda vya tumbo huambatana na maumivu ya kuchoma, kuwaka katika sehemu ya juu ya tumbo. Kwa kuwa aina mbili zote za vidonda vya tumbo hutofautiana, ni vizuri zaidi kuelezea kila kimoja. 

(a) Vidonda vya tumboni 

Maumivu ya vidonda vya tumboni mara nyingi hukaa katikati, takribani kati ya nusu ya chini na kwenye kitovu na mara nyingi kula huifanya kuwa mbaya zaidi. Tofauti na maumivu ya vidonda vya utumbo, maumivu ya vidonda vya tumbo mara nyingi hayaishi mara moja pindi yanapoanza. 

(b) Vidonda katika utumbo 

Maumivu ya vidonda vya katika utumbo pia hukaa pale pale (kama katika vidonda vya tumboni). Tofauti na vidonda vya tumboni, katika vidonda vya utumbo mara nyingi kula husaidia kupunguza maumivu. 

Tofauti nyingine ni kuwa, wakati katika vidonda vya tumboni maumivu huongezeka haraka baada ya kula chakula, katika vidonda vya utumbo inaweza kuchukua saa mbili au tatu. Tabia nyingine ya vidonda vya utumbo ni kupotea kwa majuma au hata miezi bila sababu ya wazi. 

Mtu anaweza kulalamika kuwa anapata maumivu baada ya chakula. Hii ni kutokana na msisimko wa mnyunyizo wa asidi ambao hububujika kwenye kidonda. Katika vidonda vya duodeni, huchukua takribani saa mbili hadi tatu ili asidi ifike sehemu ya kidonda. 

Utambuzi wa vidonda vya tumbo 

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hujumuisha X-Ray. Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama 'endoskopy' au 'biopsy', ambayo huyakinisha hali halisi. 

Matibabu ya vidonda vya tumbo 

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu. 

Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa muhimu. 

Katika vidonda vya tumbo ambavyo ni vikali, matibabu yake hutumia maziwa kwa mwanya wa dakika 15 hadi saa mbili kwa kutegemea ukali wa ugonjwa; kwa wiki moja. Maziwa hutumiwa pamoja na dawa. 

Maziwa si kwamba hupambana na asidi tu, bali pia huchelewesha muda wa tumbo kuruhusu dawa kufanya kazi kwa muda mrefu. Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4-6 za matibabu. 

Kuzuia mfadhaiko 

Kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara. Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa mawazo, wengine hawajui kabisa nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na mfadhaiko ambao huweza kuwasabishia maradhi kama vidonda vya tumbo au maradhi ya moyo, n.k. 

Mfadhaiko unaweza kuwa wa muda au wa kudumu. Matokeo yake yana madhara makubwa kama hautadhibitiwa. Ni vipi unaweza kudhibiti mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha? 

(a) Kuridhika na maisha 

Kama tutakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, tukaacha kuyakopa maisha ya jana na tukaacha kuhofu maisha ya kesho, hakika kabisa matumbo yetu pia yatatulia. 

Inaelezwa na wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo. Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana. 

Wasiwasi na hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa. Mvurugiko wa hisia una matokeo chanya katika kiwiliwili. Unaweza kuleta ugonjwa ambao ni wa kufisha kama ambao hutokana na lishe dhaifu. Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari, vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo. 

(b) Kutopata usingizi wa kutosha 

Ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa katika zama zetu hizi. Haraka na pilikapilika za dunia yetu ya kisasa hazina mfano. Mvurugiko wa mawazo kutokana na mwenendo wa maisha uko kila mahala. Kutokana na mahitaji ya maisha, kuna idadi kubwa ya watu ambao neva zao hazitulii. 

Kulala ni moja ya tiba za mwili. Usingizi husaga chakula na huondoa uvimbe katika tumbo, udhaifu na uchovu.

Kukesha usiku kucha husababisha kutosagika kwa chakula tumboni na hudhoofisha akili na pia husababisha akili kuvurugika. Kulala huleta pumziko kamilifu la mwili na akili. 

Madaktari wetu wanasema kuwa, kulala ni muda ambao metaboliki ya mwili hufanyika polepole kiasi kwamba sehemu kubwa ya vyanzo vyake vya nishati hupatikana kwa ajili ya makuzi ya afya njema ya mwili na akili. 

Sehemu ya kulala inatakiwa iwe ni tulivu na isiyo na kelele, pia iwe na hewa safi na asilia. Hewa asilia ina athari nzuri katika mwili wa mwanadamu, miongoni mwa athari zake ni kuiwezesha akili kufanya kazi barabara, na pia huongeza hamu ya kula. 

Kiwango cha wastani cha kulala kinachotakiwa hutegemeana na umri. Katika umri wa miaka miwili, mtu hushauriwa kulala saa 14 hadi 16 kwa siku. Miaka minne saa 12-14 kwa siku, miaka sita hadi minane saa 11-12 kwa siku, miaka minane hadi 11 saa 10-11 kwa siku, miaka 14 hadi 18 saa 8-9 kwa siku. Watu wazima wanahitaji saa za kulala kati ya sita na nane. 

http://pendo.proboards.com/index.cgi?board=healthafya&action=display&thread=34

Mambo Muhimu Ya Kufahamu Kuhusu Ukimwi

Maana ya Neno UKIMWI 

Neno UKIMWI ni kifupisho cha maneno Upungufu wa Kinga Mwilini. UKIMWI ni mkusanyiko wa magonjwa yanayotokana na kudhoofika kwa nguvu ya mwili kujikinga na magonjwa kunakosababishwa na Virusi Vya UKIMWI (VVU). 

Maana ya neno Virusi Vya UKIMWI (VVU)

Virusi Vya UKIMWI (VVU) ni vimelea vidogo vidogo vinavyodhoofisha na kufanya mwili kupoteza uwezo wa kupambana na magonjwa. Kawaida miili yetu hukingwa dhidi ya maradhi na chembechembe nyeupe za damu, lakini VVU vikiingia mwilini hushambulia chembechembe hizo na kuzipunguza. Hivyo, mwili ulioingiliwa na VVU hupungukiwa sana na chembechembe nyeupe na hukosa kinga dhidi ya maradhi. Ingawaje mara nyingi maneno haya yamekuwa yakitumika pamoja, ieleweke kwamba yana maana tofauti.

Jinsi Virusi Vya UKIMWI Vinavyoambukizwa 

Virusi Vya UKIMWI vinapatikana katika damu na majimaji mbalimbali yanayotoka kwenye mwili na viungo vya uzazi vya wanawake na wanaume wenye uambukizo. Njia kuu ya kueneza virusi hivi, hasa katika Bara la Afrika ni kujamiiana kusiko salama. Njia nyingine ni kutoka kwa mama mjamzito
mwenye Virusi Vya Ukimwi kumwambukiza mtoto wakati akiwa tumboni, anapozaliwa au wakati wa kumyonyesha. VVU pia huambukizwa kwa kuongezewa damu yenye virusi hivyo. Pia ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa kuchangia vifaa vyenye mabaki ya damu kama sindano, mikasi, wembe, mipira ya kutolea mkojo au vifaa vya kutogea masikio. 

Njia zifuatazo haziambukizi VVU 

  • Kushikana mikono na mtu mwenye VVU 
  • Kubadilishana nguo na mtu mwenye VVU ili mradi hazina majimaji au damu kutoka kwa mgonjwa wa UKIMWI 
  • Kuishi pamoja na mtu mwenye VVU 
  • Kushiriki kula chakula pamoja na mtu mwenye VVU 
  • Kugusana au kukumbatiana na mtu mwenye VVU 
  • Kushirikiana bafu na mtu mwenye VVU  
  • Kuumwa na mbu, viroboto, au wadudu wengine. 

Njia hizo zilizoorodheshwa hapo juu zisihusishe damu au majimaii mengine kutoka kwa mgonjwa wa UKIMWI 

Dalili za UKIMWI  

Hakuna njia ya hakika ya kumtambua mtu aliyeambukizwa VVU zaidi ya vipimo vya maabara. Watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI wanaweza kuonekana wazima na wasionyeshe dalili zozote za ugonjwa.  Hata hivyo pamoja na kutokuonyesha dalili zozote, mtu huyu mwenye virusi anaweza akaambukiza watu wengine ikiwa atakuwa na mahusiano yasiyo salama. 

UKIMWI ni hatua ya mwisho ya maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI.  Hatua hii ikifikiwa mwathirika huanza kushambuliwa na magonjwa mbalimbali yaitwayo magonjwa nyemelezi Dalili za UKIMWI zimegawanyika katika makundi mawili makuu:

Dalili kuu za UKIMWI 

•Kupungua uzito asilimia 10 au zaidi katika mwezi mmoja, bila sababu inayoeleweka 
•Kuharisha kwa muda mrefu  (mwezi mmoja au zaidi) 
•Homa kwa mwezi mmoja au zaidi

Dalili Ndogo za UKIMWI Utando mweupe mdomoni

•Kikohozi kwa muda wa mwezi mmoja au zaidi 
•Kupata mkanda wa jeshi (moto wa Mungu)
•Vipele sugu na vyenye kuwasha hasa mikononi na miguuni

Mgonjwa akiwa na dalili kuu tatu, au mbili kuu na ndogo mbili uwezekano wa kuwa na UKIMWI ni mkubwa. Hata hivyo vipimo zaidi vya maabara vinahitajika ili kuthibitisha kama mgonjwa ana UKIMWI.

Ugonjwa wa Hemoroid (HAENORRHOIDS) na kutokwa damu njia ya haja kubwa

TATIZO hili hujulikana pia kama ugonjwa wa vifundo katika njia ya haja kubwa. Jina jingine la ugonjwa huu ni bawasili, lakini kwa daktari bingwa wa upasuaji humaanisha matatizo katika mishipa ya damu (veins) katika njia ya haja kubwa (rectum or anus).

Hutokana na kulegea kwa misuli laini ya mishipa hiyo ya damu, hivyo mishipa kutanuka kuliko kawaida na kulegea, kisha kutokeza katika njia ya haja kubwa, ikiambatana na ukuta wa njia hiyo.

Sababu hasa ya kulegea kwa mishipa hiyo haijaweza kueleweka, lakini mabadiliko yafuatayo huchangia kwa kiasi mkikubwa.

•Kupata choo kigumu mara kwa mara

•Kuharisha mara kwa mara

•Kukaa kwa muda mrefu

•Kuwa na uzito mkubwa kuliko inavyotakiwa (BMI>30)

•Kukohoa mara kwa mara

•Uvimbe tumboni

•Kuzaa watoto wenye uzito mkubwa mfano zaidi ya kilo 4

Dalili

Kuhisi kushuka kwa fundo la sehemu ya haja kubwa wakati wa kupata choo, ambalo linaweza kurudi lenyewe ndani, baada ya kupata choo au inabidi kulirudisha kwa kidole au kushindikana kabisa kurudishwa kidole na kubaki likininng’inia nje kwa muda mrefu.

Kutokwa damu wakati wa haja kubwa ambayo huweza kuchafua nduo za ndani, wakati mwingine damu hutoka kwa wingi na mfululizo bila kuganda, hivyo kuhatarisha maisha.

Kuchafua nguo za ndani kutokana na kutokwa na majimaji sehemu za hajakubwa

Dalili nyingine ni kupatwa na maumivu makali sehemu za hajakubwa, fundo kuwa kubwa sana na kubadilika rangi, wakati damu inapokuwa imeganda ndani ya mishipa yake (thombosed prolapsed haemorrhoids)

Uchunguzi na matibabu

Ni vyema uonapo dalili hizo hapo juu uende katika hospitali iliyo karibu na kupata ushauri na matibabu ya kitaalamu zaidi.

Ni rahisi zaidi kwa daktari kuchunguza na mara moja kugundua ugojwa huu na ukubwa wa tatizo, pia kupanga njia ya matibabu. Pia lazima kuanza na vipimo vya mwanzo, mfano kupima wingi wa damu, (hemoglobin level)

Vipimo kama proctoscopy (kuchuguza kwa chombo maalumu chenye mwanga), proctosigmoidoscopy huweza kufanyika, pia kuwekewa dawa maalumu, kisha kupiga ex-ray (barium enema)

Kwa watu walio na umri mkubwa, mfano miaka 50 na zaidi ni muhimu kuchunguzwa kitaalamu zaidi, maana kundi hili lina hatari ya kupata saratani ya njia ya haja kubwa.

Hivyo, mtu anaweza kufikiri ni tatizo dogo, kumbe anasumbuliwa na saratani ya njia ya haja kubwa na hivyo matibabu hubadilika.

Ugojwa huu pia unaweza kuchanganywa na wa kushuka kwa sehemu ya utumbo na kutokeza nje ya njia ya haja kubwa (rectal prolapsed)

Matibabu

Iwapo hemoroid hazijawa kubwa sana, yaani zipo katika hatua ya kwanza au ya pili hivi, basi ni muhimu kukwepa au kutibu visababishi vinavyochochea ugonjwa kama vilivyoainishwa hapo juu. Mfano choo kigumu na kadhalika. Pia mgonjwa huweza kupewa dawa ya kulainisha sehemu ya haja kubwa.

Iwapo tatizo ni kubwa yaani lipo katika hatua ya tatu au ya nne, au matibabu tajwa hapo juu yameshindikana, basi upasuaji ndiyo matibabu sahihi ya ugonjwa huu. Upasuaji mzuri huo upo wa aina nyingi, mfano kukata au kuvifunga vifundo kwa mpira maalumu. Ifahamike kwamba mgonjwa anapokuja katika hali hatarishi kama vile vifundo kuwa na maumivu makali na kutoka damu kwa wingi (thombosed and prolapsed hemorrhoids), basi huhitajika kufanyiwa upasuaji mapema ili kumwokoa mgojwa.

Matatizo yatokanayo na ugonjwa huu

Yapo mengi, lakini kwa uchache ni kama;

•Kushindwa kupata haja kubwa katika hali ya kawaida kutokana na kupata maumivu

•Choo kuwa kigumu zaidi jinsi muda unavyokwenda na hivyo kuongeza ukubwa wa tatizo

•Kutokwa damu wakati wa kujisaidia haja kubwa

•Kutokwa damu nyingi pale hemoroidi zainapopasuka hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa

•Kuchafua nguo na kuleta adha katika jumuiya mfano kazini na majirani.

Kwa Mawasiliano 0754310407 

http://www.mwananchi.co.tz/Makala/-/1597592/1691234/-/item/0/-/h54mot/-/index.html

Uvimbe sehemu ya haja kubwa - bawasiri/bawasili (HEMORRHOIDS)

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri

Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.

Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
  • Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
  • Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
  • Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
  • Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je bawasiri husababishwa na nini?

Bawasiri husababishwa na;
  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa
Dalili za bawasiri
  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri
  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids
Vipimo na uchunguzi
  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
Matibabu

Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
Upasuaji;
  • Hemorrhoidectomy
  • Stapled hemorrhoidopexy
Njia za kuzuia Bawasiri
  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
...........................................................................................
Kuota kinyama njia ya haja kubwa

Unasumbuliwa na Kitu kinachoitwa HEMORRHOIDS na bawasili ni neno fasaha la kiswahili!bawasili inasababishwa na kupata Choo kigumu kwa muda mrefu mpaka kusababisha mishipa ya damu kutanuka kwasababu haiwi emptyed ipasavyo!hio ACOSAL ANAL ointment ni dawa sahihi kabisa au SCHERIPROCT ambayo Ina prednisolon!kama hizo dawa Njia pekee ilobakia ni upasuaji!

1. Jaribu kunywa maji ya kutosha na kula chakula chenye fiber nyingi ili uepuke kupata Choo kigumu.
2. Epuka kusimama muda mrefu au kukaa muda mrefu kama ulikuwa unafanya hivo awali
3. Fanya mazoezi ili kuongeza intenstine motility
4. Epuka kujikamua sana ukipatwa na haja kubwa

NB: Huu ugonjwa hahuhusiani na matatizo ya uzazi
......................................................................................

Haemorrhoids ni uvimbe ambao unaweza kutokea katika njia ya haja kubwa (------) na sehemu ya mwisho ya puru (rectum).
 
Kuna mtandao wa veins ndogo (mishipa ya damu) inayopita ndani ya ------ na sehemu ya chini ya rectum. Hizi veins mara nyingine zinakuwa pana na kujaa damu zaidi kuliko kawaida. Mishipa hii iliyoja damu pamoja na tishu zilizojuu yake inaweza kufanya uvimbe mmoja au zaidi uitwao haemorrhoid.

Sababu halisi kwa nini mabadiliko haya hutokea na kusababisha haemorrhoids hazijulikani. Hata hivyo, inadhaniwa kwamba shinikizo (pressure) katika ama karibu na ------ inaweza kuwa sababu kubwa katika kesi nyingi. Kama shinikizo katika ama karibu na ------ limeongezeka, basi ni wazi kwamba hii inaweza kusababisha haemorrhoids kutokea

Baadhi ya sababu zinazopelekea hali hiyo ni

-kufunga choo ama kupata choo ngumu 
-ujauzito
-sababu za kiurithi-baadhi ya watu wanaweza kuwa na kuta dhaifu

Dalili

Dalili zinaweza kutofautiana. Haemorrhoids ndogo kwa kawaida haina maumivu. Dalili ya kawaida ni kutoka damu baada ya kwenda choo. Haemorrhoids kubwa huweza kutokwa majimaji kama makamasi, maumivu kiasi, kuwasha, na kujikuna. Unaweza kuwa na hisia za haja kubwa , au hisia ya kuwa bado unahitaji kwenda haja kubwa hata baada ya kujisaidia.Wakati mwingine damu huganda kwenye haemorrhoids na hivyo huleta maumivu makali. Maumimu haya hudumu kwa siku kadhaa lakini baadae hukoma.

Matibabu

Hakikisha unapata choo la laini wakati hivyo unaweza kufanya yafuatayo.

-Kunywa maji mengi
-kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi mfano matunda mboga za majani na vyakula vya nafaka.
-Epuka dawa za maumivu zenye codaine mfano
-Nenda chooni mara tu unapohisi haja.Usijaribu kubana.

Njia hizo zote hapo juu zitasaidia kupunguza dalili mfano damu kuacha kuvuja.
Hata hivyo kuna dawa nyingine ambazo unaweza kupaka amu kuingiza kwenye ------. Dawa hizi hazimalizi tatizo bali husaidia kupunguza dalili.
Matibabu mengine ni upasuaji ambayo inaweza kuwa kufunga (banding) au kuondolewa (haemorrhoidectomy).


MAMBO 7 MUHIMU KUFANYA ILI UWE NA AFYA BORA

Yafuatayo ni baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya ili kuwa na afya bora katika mwaka huu wa 2011. Lakini kabla sijaendelea mbele sana,naomba niweke wazi kwamba afya bora haihusu kula vizuri na mazoezi peke yake bali pia fikra chanya (positive attitude). Kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba siku zote unakuwa na mawazo chanya na pia kuwa karibu zaidi na watu wenye mawazo chanya.

1. Kunywa Maji kwa wingi:

Bila shaka unakumbuka msemo “Maji ni Uhai”.Hiyo ni kweli kabisa. Maji ni uhai sio tu kwa mazingira yetu na dunia kwa ujumla bali pia kwa afya au miili yetu. Maji ni kitu muhimu sana kwa afya zetu. Asilimia 60% ya miili yetu imetengenezwa au imesheheni maji. Maji yanahitajika kwa ajili ya kuondoa takataka au vitu visivyofaa kutoka mwilini. Maji ndio hubeba virutubisho na oxygen.

Kiasi cha maji anachohitaji mtu kinategemea na mambo kadhaa kama vile unyevu (humidity) wa mahali ulipo, shughuli zinazohusisha mwili anazozifanya mtu na pia uzito wa mwili. Pamoja na hayo, kwa wastani miili yetu inahitaji lita 2 na nusu mpaka 3 za maji. Vyakula tunavyokula huchangia kama asimilia 20% za maji katika miili yetu.Kwa hiyo tunahitaji kunywa maji kiasi cha lita 2 mpaka lita 2.4 au glasi 8-9 za maji kwa siku.

Njia rahisi ya kujua kama mwili wako una maji ya kutosha ni katika kuangalia mkojo. Mkojo wako unatakiwa kutokuwa na rangi (colorless) au kuwa wa njano kidoogo. Kinyume cha hapo ni ishara kwamba hauna maji ya kutosha mwilini. Njia nyingine kutambua ni pamoja na kukaukwa na midomo (lips) na hata ulimi na pia kupata kiasi kiduchu cha mkojo.

2. Pata Usingizi wa Kutosha: 

Unakumbuka tulipokuwa wadogo wazazi wetu walisisitiza sana kwamba twende tukalale mapema ili tukue? Bila shaka walikuwa wanajua kwamba usingizi ni sehemu muhimu sana katika afya. Ukiachilia mbali faida za usingizi kwa ajili ya afya za akili/ubongo wetu, usingizi au mapumziko ya kutosha ni muhimu kwa miili.Afya njema huenda sambamba na mapumziko. Ni wakati wa kuupa mwili nafasi ya kujijenga, kujiongezea nguvu na muhimu zaidi kuhakikisha kwamba tunakuwa na akili timamu. Pia ukosefu wa usingizi ni chanzo cha kuzeeka mapema.

3. Fanya Mazoezi: 

Hili linaweza kupita bila maelezo ya ziada.Mazoezi ni muhimu sana kwa afya bora. Fanya mazoezi angalau mara tatu katika wiki. Jipatie muda wa kutembea japo kwa dakika 30. Kama inawezekana nenda Gym. Badala ya kupanda lifti pale kazini kwako au mitaani, tumia ngazi za kawaida. Egesha gari lako mbali kidogo na unapokwenda ili upate nafasi ya kutembea nk. Muhimu zaidi ni kuchagua aina ya mazoezi unayoipendelea. Mazoezi hayatakiwi kuwa adhabu.

Faida za mazoezi ni pamoja na kujiepusha na magonjwa mbalimbali, kupunguza unene (bila shaka unajua kwamba unene kupindukia sio afya bali ni ugonjwa na sababu kubwa ya maradhi mengine)

4. Kula Matunda Kwa Wingi: 

Matunda ni chanzo kizuri sana cha madini na vitamins ambazo miili yetu inahitaji sana kwa ajili ya afya bora. Unajua kwamba machungwa,kwa mfano, yana faida kubwa zaidi kiafya kuliko vidonge vya Vitamin C unavyobugia kila leo? Aina mbalimbali za matunda ambayo yana virutubishi vingi zaidi kiafya ni Parachichi(Avocado), apple, matikiti maji (cantaloupe), Zabibu (Grapefruit), Kiwi, Guava, mapapai, machungwa, strawberries nk.

5. Kula mboga za majani:

Kama ilivyo kwa matunda, mboga za majani (vegetables) ni muhimu sana kwa afya zetu. Wataalamu wa afya wanashauri kwamba tule aina 5 mpaka 9 za mboga za majani na matunda. Jitahidi kupata angalau zaidi ya aina 5 za mboga za majani na matunda.

6. Punguza Kula Vyakula vya Makopo:

Kutokana na jinsi dunia inavyozidi kwenda mbio,watu wengi huwa tunakosa muda wa kupika.Matokeo yake tunakimbilia kwenye vyakula vya kwenye makopo ambavyo ndivyo vimejaa katika maduka na ma-supermarket. Jitahidi kuviepuka vyakula hivyo kwa kadri unavyoweza.Mara nyingi vyakula vya makopo huwa na ingredients ambazo hazifai kwa afya zetu. Kwa mfano, vingi miongoni mwa vyakula hivyo huwa na chumvi nyingi kitu ambacho ni chanzo cha High Blood Pressure na maradhi ya moyo. Unaposhindwa kabisa kujizuia kununua vyakula hivyo vya makopo jaribu kuangalia ambavyo havina sukari au chumvi.

7. Jipende:  

Kama nilivyodokeza hapo mwanzo, afya bora huenda sambamba na afya ya akili/ubongo. Njia mojawapo ya kupata afya hiyo ni pamoja na kujipenda. Pengine unajiuliza, kuna mtu ambaye hajipendi? Ukweli ni kwamba pengine ni kweli kwamba hakuna mtu ambaye hajipendi.Tofauti inakuja pale mtu anapofanya vitu ambavyo ni kinyume kabisa na mapenzi ya mwili. Mfano, uvutaji sigara, unywaji pombe kupindukia,  kutojisafisha mwili wako kwa mfano kuoga, kupiga mswaki na pia kupumzika nk. Hizo zote ni tabia ambazo zinaweza kuonyesha jinsi ambavyo hujipendi au huupendi mwili wako. Kama unaupenda utautumia vibaya au kuuharibu?

AFYA YA NGOZI: Mba na madhara yake mwilini-2

Kama tulivyoeleza wiki jana, hamira ni jamii ya fangasi ambao hushambulia mwili. Mba ni jamii hiyo.

Je, ni vipi hushambulia ngozi?

Maeneo yenye mabaka yanayoletwa na fangasi wa aina hii hubadilika rangi yake na kuwa na rangi hafifu au inayoonekana zaidi (kama ni mtu mwenye rangi ya maji ya kunde basi ngozi iliyoathiriwa hubadilika na kuwa nyeupe au nyeusi sana.

Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi wa aina hii kusimamisha shughuli za uzalishaji wa homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.

Upungufu huo ya rangi ya ngozi si wa kudumu, bali ngozi hurudi kwenye hali ya kawaida ya rangi yake baada ya muda mrefu kidogo tangu maradhi halisi yalipokomeshwa. Bila matibabu maradhi haya huchukua muda kupona hivyo dawa ni muhimu ili mwenye maradhi aweze kupona upesi.

Namna ya kuyatambua

Maradhi haya ni rahisi  kuyagundua ila kutokana na kufanana kwake na maradhi mengine yenye dalili kama hizi uhakiki wa vimelea vinavyosababisha maradhi haya ni muhimu.

Sehemu ya ngozi kutoka kwenye eneo lenye maambukizi huchukuliwa na kupelekwa maabara ambako sehemu hii ya ngozi huwekwa kwenye darubini maalum kwa ajili ya kuangalia vimelea hivi vya fangasi.

Nini matibabu yake?

Maradhi haya huweza kutibika kirahisi, ila mara nyingi hurudia kushambulia ngozi hasa eneo ambalo liliwahi kushambuliwa kabla.

Kutokana na uwezo wake wa kurudia kuambukiza ngozi huwa inashauriwa kwa aliyewahi kupata maradhi haya kurudia kutumia dawa ya kuua vimelea vya fangasi mara kwa mara ili kuondoa uwezekano wowote wa maradhi kurudia kushambulia. 

Matibabu ya maradhi haya huhusisha dawa za kupaka zinazoua vimelea hivi vya fangasi.

Dawa za kuua vimelea vya fangasi za kunywa pia hutolewa kwa ajili ya kutibu aina hii ya fangasi lakini hushauriwa zitolewe tu kama dawa za kupaka zimeshindwa kuua vimelea hivi vya fangasi. 

Maradhi yanayofana nayo:

Kuna magonjwa ambayo hufanana na maradhi haya. Mfano ;

-Pumu ya ngozi

-Vitiligo

Maradhi haya tutayazungumzia kwenye makala zijazo kwenye mtiririko huu.

Matokeo baada ya matibabu

Kama nilivyoandika hapo juu maeneo ya ngozi yaliyobadilika rangi huweza kubaki hivyo hata baada ya vimelea vya fangasi kuondolewa na dawa.

Hii inamaanisha inawezekana kabisa mgonjwa akabaki na mabaka yanayotokana na vimelea hivi vya fangasi muda mrefu hata baada ya kutumia dawa ambayo imefanikiwa kuondoa vimelea hivi vya fangasi.  Hali hii mara nyingi huchanganya wagonjwa na kusababisha wagonjwa kudhani kuwa maradhi bado upo hivyo kuendelea kutumia dawa au kuanza kutumia dawa baada ya muda mfupi tangu kumaliza kutumia dawa zilizofanikisha uondoaji wa vimelea.

Hali ya sehemu ya ngozi iliyoathiriwa na vimelea vya fangasi kurudisha rangi ya kawaida ya ngozi kama sehemu nyingine ambazo hazikua na madhara huchukua muda mrefu kidogo ingawa kama eneo husika lilikua na uvimbe basi uvimbe hupotea haraka.

http://www.mwananchi.co.tz/AFYA-YA-NGOZI---Mba-na-madhara-yake-mwilini-2/-/1596774/1964932/-/ccojj2z/-/index.html

Matumaini ya Chanjo ya Malaria 2015

Kampuni ya kutengeza madawa ya GlaxoSmithKline inataka kuruhusiwa kisheria kuidhinisha chanjo ya kwanza ya Malalaria ikisema kuwa imeweza kupunguza vifo vya Malaria miongoni mwa watoto barani Afrika.
....................
Wataalamu wanasema kuwa wana matumaini kuhusu mafanikio ya chanjo hiyo ya kwanza ya Malaria duniani baada ya kufanyiwa majaribio.

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na Mbu na ambao huwaua maelfu ya watu duniani kila mwaka.

Wanasayansi wanasema kuwa chanjo inayofaa ndio njia ya pekee kumaliza ugonjwa wa Malaria.

Chanjo hiyo inayojulikana kama RTS,S iligunduliwa kuwa iliweza kupunguza idadi ya vifo vya Malaria miongoni mwa watoto wadogo wakati wa majiribio na pia iliweza kupunguza vifo miongoni mwa watoto wachanga kwa 25% .

Kampuni ya GlaxoSmithKline (GSK) inatengeza chanjo hiyo kwa usaidizi wa wakfu wa Bill na Melinda Gates.

Majaribio ya chanjo yenyewe yalifanyiwa barani Afrika ambako iliwahusisha watoto 15,500 kutoka nchi saba.

Matokeo yaliwasilishwa kwenye mkutano wa matibabu uliofanyika mjini Durban, Afrika Kusini.

Kampuni ya GlaxoSmithKline sasa inataka kisheria iweze kuruhusiwa kuanza kuuza chanjo hiyo ambayo imekuwa ikitengezwa kwa miongo mitatu.

Kwa mujibu wa kampuini hiyo, inataka shirika la afya duniani kuweza kuidhinisha matumizi ya RTS,S angalau kuanzia mwaka 2015 ikiwa wadhibiti wa madawa EMA wanaweza kuwapa leseni ya kuanza kuuza chanjo hiyo.

Kulingana na utafiti uliofanyiwa watoto waliopewa chanjo hiyo, ulionyesha kuwa miezi 18 baada ya kupewa chanjo watoto waliona miezi mitano hadi 17 waliweza kukingwa dhidi ya ugonjwa huo kwa 46% .Lakini watoto waliokuwa kati ya wiki 12 wakati huo waliweza kukingwa tu kwa asilimia 27.

Msemaji wa kampuni ya GSK, aliambia shirika la habari la AFP kuwa kampuni itawasilisha ombi lake chini ya mkakati wa kuziwezesha nchi maskini kuweza kupata dawa.

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2013/10/131008_malaria_chanjo.shtml